Bocco aita mashabiki uwanja wa Taifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Mar 2018
Bocco aita mashabiki uwanja wa Taifa
Nahodha wa timu ya Simba John Bocco amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kesho Jumatano kuipa sapoti Simba itakapokwaana na Al Masry kwenye mchezo wa kombe la shirikisho, raundi ya kwanza.

Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari leo kuelekea mchezo huo, Bocco amesema ari ya wachezaji iko juu na wako tayari kuikabili Al Masry.

"Tumejiandaa vizuri, wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo wa kesho. Tunawaambia Watanzania waje kwa wingi uwanja wa Taifa kutupa sapoti," amesema Bocco.

Naye kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre amesema ana uzoefu wa kukutana na timu za Misri hivyo amewatoa hofu mashabiki wa Simba.

Lechantre amesema Simba itacheza mchezo wa Kimataifa kesho na watahakikisha wanaanza vyema kwa kuibuka na ushindi nyumbani.

Afisa habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki waendelee kununua tiketi kwa wingi wakati huu ili wasipate tabu hapo kesho.

Aidha, Manara amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho..

Manara ameeleza kuwa anatambua mchango wa mashabiki hivyo vema wakaja kwa wingi uwanjani ili kuipa hamasa timu na wachezaji kwa ujumla.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12:00 jioni ambapo viingilio vitakuwa; VIP A 20,000/- VIP B na C 15,000/- na mzunguuko 5,000/-
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
16h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
20h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’