Baada ya Vodacom kujitoa, TPLB yasaka wadhamini wapya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Jun 2021
Baada ya Vodacom kujitoa, TPLB yasaka wadhamini wapya

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL) imesema kwa sasa inasaka wadhamini wengine baada ya Kampuni ya Vodacom kutangaza kujitoa

Vodacom wametakiwa kumalizia kiasi cha fedha wanachodaiwa na klabu zinazoshiriki ligi hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almas Kasongo alisema taarifa ya Kampuni ya Vodacom kujitoa Ligi Kuu walikuwa nayo tangu mwaka jana na walishaanza vikao vya ndani na sasa wanatafuta mdhamini mwingine.

Kasongo alidai kampuni hiyo ilishindwa kutimiza makubaliano ya kimkataba ya kutoa Sh bilioni 3 kwa msimu na kuja na mapendekezo ya kutoa Sh milioni 500 na kuahidi fedha iliyobaki sawa na Sh bilioni 2.5 kulipa katika msimu wa 2022/23 wakati mkataba wao unamalizika msimu wa 2021/22.

"TPLB iliwaomba Vodacom kutoa Sh milioni 600 ambayo ni robo ya Sh bilioni 3 za kwenye mkataba na klabu zilikubali mapendekezo hayo, ambayo yalikuwa siri kutokana na siri hiyo kuvuja milango ipo wazi kwa mdhamini mwingine," alisema Kasongo

Alisema katika barua yao ya Agosti walisema hawawezi kutimiza yale waliyokubaliana kwenye mkataba, kwani kila msimu walitakiwa kutoa Sh bilioni 3 na katika makubaliano wanadaiwa Sh bilioni 2.5 kutokana na changamoto zinazowakabili na waliwakubalia

Kasongo alisema hizo ni fedha za klabu na watakapozilipa watazipeleka kwenye klabu maana walipojulishwa changamoto zinazoikabili kampuni hiyo walikubali kuwavumilia maana kuanzia waanze kudhamini ligi hiyo hawajawahi kukwama.

Awali, Vodacom walisaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh bilioni 9, ambapo kila mwaka walitakiwa kutoa Sh bilioni 3.

Juni 6, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hisham Hendi alisema imekuwa ni fahari kubwa kwao kudhamini Ligi Kuu Tanzania kwa kipindi cha miaka 10.

Lakini kutokana na mwenendo wa ufanisi wa kampuni hawataendelea

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
11h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
11h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
14h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’