Pamoja na kuhusishwa kumuwania mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata, hizo zitabaki kuwa tetesi tu kwani inaelezwa mabingwa wa nchi Simba wamemuongezea mkataba mlinda lango namba mbili Beno Kakolanya
Msimu ujao Simba itaendelea na walinda lango wake watatu, Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ali Salim
Awali kulikuwa na presha kwa Manula aliyekuwa akiwaniwa na timu kadhaa kutoka nje ya nchi
Hata hivyo Kocha Didier Gomes amegomea Manula kuuzwa akiwa miongoni mwa wachezaji 17 ambao amewahitaji kwa ajili ya mipango yake ya msimu ujao
Katika hatua nyingine, Simba imekamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto Edward Charles Manyama aliyesajiliwa kutoka klabu ya Ruvu Shooting
Manyama anasubiri utambulisha tu wakati ukifikaΒ
ADVERTISE HERE