Tayari kinadada wa Simba Queens 'wameshasepa' na ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake kwa msimu wa pili mfululizo
Aidha kaka zao Simba Sc waliojipambanua kuwa wababe wa soka Tanzania, wanahesabu siku tu kabla ya kushangilia ubingwa wa nne mfululizo VPL
Wamebaki vijana wa U20 ambao nao walifanikiwa kutinga hatua ya nane bora ligi kuu ya vijana inayotarajiwa kuanza kesho Alhamisi
Mchezo wa kwanza wanaanza na watani zao Yanga mchezo ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex 'Chamazi'
Mpango wa Simba ni kushinda makombe yote ambayo timu zake zinashiriki msimu huu huku msemaji wa mabingwa hao wa nchi Haji Manara akitamba kuwa watafanya hivyo kwa miaka 10
Msimu uliopita vijana hawakufanya vizuri sana wakipoteza mchezo dhidi ya watani zao Yanga kwenye dakika za majeruhi
Lakini msimu huu kikosi kiko imara na wameahidi wanaanza na alama tatu katika mchezo dhidi ya Yanga