Mlinzi wa kushoto wa Ruvu Shooting Edward Charles Manyama anatajwa kumalizana na mabingwa wa nchi Simba
Manyama ameonyesha kiwango kizuri tangu alipokuwa na klabu ya Namungo Fc kabla ya kujiunga na Ruvu Shooting kwenye usajili wa dirisha dogo mwaka huu
Ni usajili utakaoweka matatani hatma ya Gadiel Michael ambaye hana wakati mzuri ndani ya kikosi cha Simba
Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' ametumika zaidi kwa kuwa hapati upinzani mkali kutoka kwa Gadiel aliyesajiliwa kutoka klabu ya Yanga mwaka juzi
Kama Simba itamsajili Manyama basi ni wazi Gadiel hatakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Gomes msimu ujao
ADVERTISE HERE