Kikosi cha Simba jana kilifanya mazoezi usiku kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry utakaopigwa uwanja wa Taifa kesho Jumatano.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12 jioni, hivyo kufanya mazoezi usiku ni sehemu ya maandalizi ya kuwa tayari kucheza kikamilifu kulingana na wakati wa mchezo huo.
Katika mazoezi ya jana, nahodha John Bocco na Emanuel Okwi walishiriki kikamilifu huku kiungo Haruna Niyonzima aliyerejea mwishoni mwa wiki kutoka India, alirejea kikosini na kwa mara ya kwanza kufanya mazoezi na wachezaji wengine.
Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri. Baadae kocha Mkuu Pierre Lechantre anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari.

ADVERTISE HERE