Gomes aanza hesabu za msimu ujao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jun 2021
Gomes aanza hesabu za msimu ujao

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes kwa sasa hesabu zake ni kuelekea msimu ujao baada ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu pamoja na kutetea kombe la FA

Simba imesalia na michezo saba kumaliza msimu wa VPL, lakini Wekundu hao wa Msimbazi wanahitaji kushinda michezo mitatu tu kulirejesha taji kabatini pale Msimbazi kwa msimu wa nne mfululizo

Kwenye kombe la FA mabingwa hao watetezi wameingia nusu fainali mchezo wa hatua hiyo ukiwa dhidi ya Azam Fc

Gomes amesema kwa mtizamo wake ni kuwa msimu huu umemalizika na sasa wameanza maandalizi kuelekea msimu ujao

"Tumebakiwa na michezo saba kabla ya kumaliza msimu, kwa ubora tuliokuwa nao hivi sasa ukilinganisha na ule wa wapinzani wetu naona kama ligi imekwisha na Simba ndio bingwa hata kwenye Kombe la FA bado sijaona timu ambayo itatuzuia kutetea taji hilo," alisema Gomes ambaye hivi karibuni alisafiri kwenda Ufaransa kwa ajili ya mapumziko

Kocha huyo mwenye uzoefu wa soka la Afrika, amesema sasa yupo katika mazungumzo muhimu na uongozi wake kuhusu kukiboresha kikosi na aina ya wachezaji ambao wamepanga kuwaongeza ambao uwezo wao utakuwa tofauti kutokana na malengo waliyokuwa nayo

Alisema mafanikio waliyoyapa msimu huu yanahitaji juhudi kuyaendeleza msimu ujao na hiyo inahitaji umakini mkubwa, hasa katika kipengele cha usajili, ambacho ndio chenye kuonesha ubora wa timu na upatikanaji wa matokeo mazuri.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’