Baada ya mapumziko ya siku nne, kikosi cha Simba leo kimerejea mazoezini kujiandaa na michezo ya lala salama kukamilisha msimu ambapo Juni 19 watakuwa mkoani Mwanza kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba
Simba imerejea mazoezini leo uwanja wa Mo Simba Arena kikosi kikiwajumuisha wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa na wale waliokuwa majeruhi
Mazoezi yanafanyika chini ya kocha wa viungo Adel Zrane ambaye anawarudisha wachezaji katika hali ya kimichezo baada ya kutoka mapumziko
Aidha uongozi wa Simba unakusudia kuandaa mechi kadhaa za kirafiki kabla ya ligi kurejea
ADVERTISE HERE