Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere amekanusha tetesi zilizotolewa na Wakala wake Patrick Gakumba kuhusu hatma yake ndani ya Msimbazi
Kagere amesema kwa sasa hamtambui wakala huyo kwani hana mkataba wowote na Wakala yeyote wa mpira wa miguu
Kagere ametoa kauli hiyo baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Gakumba amedai kuwa mkataba wa Kagere na Simba unamalizika hivyo anazikaribisha mezani timu zinazomuhitaji

Akiwa nchini Rwanda kwa ajili ya majukumu ya Kimataifa, Kagere amesema bado ana mkataba na Simba na kwa sasa akili yake ni katika kuwatumikia mabingwa hao wa nchi
"Mimi nina mkataba na Simba, nimetuliza akili yangu katika kuitumikia Simba. Sina mkataba na wakala yeyote wa mpira wa miguu," Kagere alikaririwa media nchini Rwanda
Hivi karibuni Gakumba aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Simba baada ya kumtuhumu kocha Didier Gomes kuwa hamtumii Kagere kutokana na sababu binafsi
Uongozi wa klabu ya Simba ulimkemea Gakumba aache kuingilia masuala ya benchi la ufundi kwani hayamuhusu