Klabu ya Simba imetuma wawakilishi mkoani Mtwara ambao watakuwa na jukumu la kusaka vipaji vya wachezaji katika mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA yanayofanyika mkoani humo
Simba imeanza program maalum za kutengeneza timu za vijana ambazo baadae zitakuwa kitovu cha kupatikana wachezaji watakaoitumikia Simba baadae
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Simba imetoa taarifa hii;
"Klabu ya Simba tunaipongeza na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita kwa kutambua mizizi ya vipaji na kurejesha mashindano ya michezo mashuleni ambayo ni Umiseta na Umitashumta.
"Klabu ya Simba imetuma wawakilishi wake (Scouts) katika michuano hiyo ambayo kitaifa inafanyika mkoani Mtwara Juni hadi Julai mwaka huu kutafuta vipaji vya kesho na keshokutwa vitakavyovaa jezi yetu ya Simba.
"Huu ni mwanzo tu wa mchakato wetu wa kuweka programu madhubuti ya timu zetu za vijana. Tutashiriki kikamilifu Mtwara 2021"