Simba U20 uso kwa uso na Yanga U20 ligi ya vijana

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Jun 2021
Simba U20 uso kwa uso na Yanga U20 ligi ya vijana

Timu za vijana za Simba na Yanga zitapambana Juni 10 katika awamu ya pili ya Ligi Kuu ya vijana chini ya miaka 20 katika mchezo utakoafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi

Timu hizo zimepangwa kundi moja katika mkondo wa pili wa mechi zitakazoanza Juni 10 hadi 19 kwenye uwanja wa Azam Complex

Timu nane zimefuzu mkondo wa pili baada ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi ya mechi ambazo zilikua zinachezwa kwa muundo wa mechi za nyumbani na ugenini

Simba imepangwa kundi A pamoja na watani zao Yanga, pia zimo Mwadui Fc na JKT Tanzania

Kundi B lina timu za Prisons, Azam Fc, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar

Michezo ya nusu fainali itapigwa Juni 17 ambapo itajumuisha timu zilizomaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili wakati mchezo wa fainali utapigwa Juni 19 kumpata bingwa wa ligi kuu ya vijana kwa msimu huu

Simba imedhamiria kushinda makombe yote ambayo timu zake zinashiriki

Tayari Simba Queens wameshinda taji la ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' wakati Wanaume wakihesabu siku kabla ya kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa nne mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’