Mkurugenzi Mtendaji wa Simba SC, Barbara Gonzalez amefichua sababu ya mabingwa hao wa nchi kuonekana kuwa hawazuiliki katika harakati zao za kushinda taji la ligi kuu 2020-21
Miamba hiyo ya Msimbazi ilikuwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza siku ya Alhamisi wakati ikiisambaratisha Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mechi ambayo ilishuhudia mshambuliaji John Bocco akifunga mabao mawili na Chris Mugalu kuongeza la tatu.
Kufuatia ushindi huo, Simba ilifikisha alama 67 juu kileleni mwa msimamo wa ligi, na kuongeza tofauti ya alama sita dhidi ya Yanga inayoshika nafasi ya pili
Mchezo huo ulikuwa wa saba mfululizo kwa Simba kushinda kwenye ligi
Gonzalez amesema makali ya timu hiyo yanasukumwa na ukweli kwamba wachezaji wana hamu ya kushinda taji hilo ili kuandika historia kwa kulishinda mara nne mfululizo.
"Ni hisia hiyo ya kushinda taji tena ambayo inasukuma timu kupata matokeo mazuri," Gonzalez aliuambia mtandao wa Goal
"Wachezaji wameamua kuhakikisha wanatawazwa mabingwa na kwa hivyo hawataki kufanya makosa yoyote, wanajua jinsi ilivyo ngumu kuwa bingwa, kwa hivyo wachezaji wameamua kupambana hadi mwisho"