Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu klabu ya Simba Suleiman Kova amesema leo watamuhoji kiungo Jonas Mkude anayekabiliwa na makosa ya utovu wa nidhamu
Ni makosa yanayojirudia kwa Mkude hii ikiwa mara ya pili mwaka huu kwa nyota huyo kufikishwa mbele ya Kamati hiyo
Kova amesema wao kama kamati wanatimiza wajibu wao bila ya kujali ni mara ngapi nyota huyo amefikishwa mbele ya kamati yao
Ni wazi Mkude anaendelea kujiweka matatani licha ya kuwa ni mchezaji mwandamizi zaidi ndani ya kikosi cha Simba
ADVERTISE HERE