Kiungo Mkenya Francis Kahata anatarajiwa kuondoka nchini kurejea kwao baada ya mkataba wake na Simba kumalizika
Baada ya usajlli wa Perfect Chikwende kwenye dirisha dogo, Kahata alibadilishiwa majukumu ndani ya kikosi
Kahata aliyekuwa amebaki na mkataba wa miezi sita wakati huo, alijumuishwa katika kikosi kilichokuwa kinashiriki ligi ya mabingwa pekee
Baada ya Simba kutolewa, nyota huyo amebaki bila jukumu lolote huku Simba ikiwa haijafanya nae mazungumzo ya kumuongezea mkataba
Kahata alijiunga na Simba msimu wa 2018/19 akitokea klabu ya Gor Mahia
Ameitumikia Simba kwa misimu miwili, akifanya vizuri zaidi katika msimu wake wa kwanza kabla ya kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza
ADVERTISE HERE