Nahodha wa Simba John Bocco amesema kwa sasa lengo la kwanza ni kuisaidia Simba kuweza kushinda ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo
Jana Bocco alifunga mabao mawili wakati Simba ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba
Amefikisha mabao 13 akiwa nyuma kwa tofauti ya bao moja dhidi ya Prince Dube wa Azam Fc mwenye mabao 14 katika kinyan'ganyiro cha kuwania ufungaji bora
Hata hivyo Bocco amesema hafikirii tuzo ya ufungaji bora, kwa sasa jambo muhimu kwake ni kuona Simba inashinda ubingwa
"Kwa sasa naangalia zaidi kuisaidia timu yangu iweze kutetea ubingwa, sio ufungaji bora. Lakini kama itatokea nitaibuka mfungaji bora nitafurahi lakini sio kipaumbele changu," alisema Bocco
Bocco ameweka rekodi ya kipekee katika ligi kuu ya Vodacom akifunga mabao zaidi ya 10 katika misimu saba mfululizo
Katika misimu hiyo saba, Bocco amefunga mabao 100!