Kabla ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Simba wameshinda mabao 3-0, wachezaji wa Simba walionyesha umoja wao kwa kumfariji kiungo Clatous Chama ambaye mwishoni mwa wiki alipata msiba wa kufiwa na mkewe
Aidha Klabu ya Simba iliwakilishwa na Mr Ally Shatry msaidizi wa Afisa Habari kwenye msiba huo ulifanyika Kitwe nchini Zambia

Mwakilishi huyo aliwasilisha rambirambi za awali kwa familia ya Chama
Chama ametoa shukrani za kipekee kwa Mtendaji Mkuu, Menejimenti, Bodi ya Wakurugenzi, Wanachama na Mashabiki wote wa Simba kwa salamu zao za pole na kuomba wazidi kumuombea yeye na familia yake ili wapate nguvu zaidi
ADVERTISE HERE