FT : Ruvu Shooting 0-3 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jun 2021
FT : Ruvu Shooting 0-3 Simba

Ruvu Shooting wametepeta mbele ya Simba leo baada ya kufumuliwa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Hii ndio Simba ambayo ikiwa na jambo lake hakuna wa kuizuia!

Ushindi wa bao 1-0 waliopata katika mchezo wa duru ya kwanza, uliwapa kiburi Ruvu shooting Msemaji wao Masau Bwire akitamba kila kona

Lakini leo baada ya dakika 90 kukamilika, Bwire ilimlazimu kutafuta kichaka cha kujificha kwani maji ya shingo

Mabingwa wa nchi Simba walitawala mchezo huo tangu dakika ya kwanza, wakaandika bao la kuongoza mapema tu kwenye dakika ya 17 kupitia kwa nahodha John Bocco

Ilikuwa siku nzuri kwa Bocco kwani muda mfupi kuelekea mchezo huo alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Simba mwezi Mei

Chris Mugalu ameendeleza pale alipoishia mchezo uliopita akiifungia Simba bao la pili kupitia pasi murua ya Bernard Morrison 'Mzee wa kuwakera'

Morrison aliisaidia Simba kupata mkwaju wa penati kwenye dakika za majeruhi baada ya kufanyiwa madhambi na mlinda lango wa Ruvu Shooting

Bocco akitumia nafasi hiyo kuifungia Simba bao la tatu likiwa ni bao lake la pili siku ya leo

Ruvu Shooting walimaliza tisa baada ya wachezaji wake wawili kutolewa nje kwa kadi nyekundu

Juma Nyosso alimpiga ngumi Shomari Kapombe wakati mlinda lango alitolewa baada ya kumfanyia madhambi Morrison

Simba imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 67

Alama tisa zimesalia kabla ya Simba kushangilia ubingwa wa msimu wa nne mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’