Mabingwa wana jambo lao CCM Kirumba dhidi ya Ruvu Shooting

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jun 2021
Mabingwa wana jambo lao CCM Kirumba dhidi ya Ruvu Shooting

Mabingwa wa nchi Simba jioni ya leo watashuka uwanja wa CCM Kirumba kuwakabili maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Huu ni mchezo wa duru ya pili baina ya timu hizo msimu huu huku Ruvu Shooting wakiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 katika mchezo wa duru ya kwanza

Hata hivyo leo wanakutana na Simba nyingine kabisa, Simba ya Didier Gomes ambayo haijapoteza mchezo wowote kwenye ligi tangu kocha huyo alipotua nchini mwanzoni mwa mwezi Januari 2021

Hesabu za 'Mnyama' ni kushangilia ubingwa mapema, wanahitaji kushinda mechi nne tu

Ushindi dhidi ya Ruvu leo utawafanya waendelee kusogea karibu ya ubingwa kwa mara ya nne mfululizo

Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliopita, Simba imepania kuendeleza wimbi la ushindi pale CCM Kirumba

Kocha Msaidizi Selemani Matola amesema baadhi ya wachezaji watakosekana kutokana na sababu mbalimbali

Joash Onyango ni majeruhi wakati Clatous Chama yuko Zambia anakohudhuria msiba wa mkewe aliyefikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita

Simba ilitua jijini Mwanza ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 ambao leo wana jukumu la kuwapa furaha Wanamsimbazi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
38m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’