Simba imepania kulipa kisasi dhidi ya Ruvu Shooting

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jun 2021
Simba imepania kulipa kisasi dhidi ya Ruvu Shooting

Mabingwa wa nchi Simba wako jijini Mwanza ambapo siku ya kesho Alhamisi, watashuka katika uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Ruvu Shooting ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Jana jioni Simba ilifanya mazoezi uwanja wa Nyamagana kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu mashabiki wa Simba jijini Mwanza na kote nchini

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wote 21 waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo wako tayari kuwapa furaha Wanamsimbazi siku ya kesho

Aidha Mkufunzi wa Simba Didier Gomes amesema anafahamu wanakutana na timu ambayo iliwafunga katika mchezo wa duru ya kwanza, lakini hawataruhusu jambo hilo litokee tena

"Hautakuwa mchezo mwepesi, Ruvu Shooting ni timu nzuri, wana wachezaji wazuri lakini kwa upande wetu tumejiandaa vizuri na lengo letu ni kushinda kila mchezo unaokuja mbele yetu ili tuweze kutetea ubingwa," alisema Gomes

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’