Morrison bado 'anawakera' Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jun 2021
Morrison bado 'anawakera' Yanga

Imekuwa kawaida wa viongozi wa Yanga kuibuka kila wakati winga Bernard Morrison anapofanya tukio

Wapo waliotabiri kuwa baada ya kufunga bao la 'kideo' kule Ruangwa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc, Yanga wangefufua kesi dhidi yake!

Ndicho kilichotokea kwani jana Yanga walidai kesi ya nyota huyo itaunguruma CAS kuanzia Juni 02 ingawa ukiingia kwenye tovuti ya CAS katika tarehe hiyo hakuna kesi yoyote kutoka Tanzania

Uzuri kesi zote zinazosikilizwa, taarifa zake zinawekwa katika mtandao rasmi wa Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo

Lakini pia wapo wanaohusisha kuibuliwa kwa kesi hiyo na jaribio la kuzima wanaohoji kuondoka kwa mchezaji wao Carlinhos ambaye amevunja mkataba na 'kusepa' zake kwao jana

Kila mambo yanapochafuka, utasikia linaibuliwa jambo. Morrison ametumika kila wakati kuficha madhaifu, lakini ukweli unajulikana, Morrison ni mchezaji halali wa Simba

Kungekuwa na tatizo asingepewa vibali vyote vya kuitumikia Simba kwenye ligi ya ndani na hata michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Acha hizi 'sarakasi' ziendelee lakini mwisho wake unakaribia, wanaotumia shauri la Morrison kujificha, wataumbuka

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
52m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’