Mshambuliaji Emmanuel Okwi hivi karibuni aliteuliwa kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Uganda akichuku nafasi ya Denis Onyango aliyetangaza kustaafu kuichezea timu ya Taifa
Katika taarifa rasmi ya majukumu yake hayo mapya ambayo aliiweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, baadhi ya wachezaji wa Simba waliweka ujumbe wa kumpongeza huku wengine wakidokeza kuwa wanamsubiri ajiunge nao
Okwi anakipiga na klabu ya Al Ittihad Alexandria Club inayoshiriki ligi kuu ya Misri
Alisajiliwa na timu hiyo mwaka juzi kwa mkataba wa miaka miwili
Maana yake ni kuwa Okwi atakuwa mchezaji huru kuanzia mwezi Julai
Pengine ni nafasi nyingine kwake kurejea Msimbazi kwa mara ya tatu
Okwi amejipambanua kuwa Mwanafamilia wa klabu ya Simba, haitakuwa ajabu kumuona akirejea kwa mara nyingine Msimbazi