Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi mkoani Mtwara kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Juni 03 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Huu ni mchezo muhimu kwa Simba katika kampeni yake ya kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo
Kimahesabu, Simba inahitaji kushinda michezo minne ili kutwaa ubingwa mapema tu
Lakini pia hawa Ruvu Shooting wana kesi na Mnyama, mchezo wa duru ya kwanza walipata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Hivyo huu utakuwa mchezo wa kisasi kwa Simba ambayo imetokea kule Ruangwa kuwaadhibu Namungo Fc kwa kuwachapa mabao 3-1
Kocha Didier Gomes ameamua kukiandaa kikosi chake mkoani Mtwara kabla ya kuianza safari ya jijini Mwanza
ADVERTISE HERE