Kwa msimu wa nne mfululizo safu ya ushambuliaji ya Simba imeendelea kutamba kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara
Msimu huu Simba inakimbiza VPL kwa kufunga mabao mengi (61) pia kuruhusu mabao machache (11)
Katika hayo mabao 61, mabao 45 yawekekwa kambani na wachezaji watano tu
Meddie Kagere na John Bocco ndio vinara kila mmoja akiwa amefunga mabao 11
Mcongomani Chris Mugalu anafuatia akiwa ameweka kambani mabao 9
Luis Miquissone na Clatous Chama ndio wachezaji hatari zaidi kwani pamoja na kila mmoja kufunga mabao saba, wamechangia mabao mengine 22
Chama ametoa usaidizi katika mabao 13 wakati Miquissone amesaidia mabao tisa
Hakika hizi ni rekodi za kutisha ambazo 'Mnyama' anaendelea kuzitengeneza
ADVERTISE HERE