Kiungo Francis Kahata alibadilishiwa majukumu ndani ya klabu ya Simba katika usajili wa dirisha dogo akisajiliwa kwa ajili ya mechi za Kimataifa tu
Baada ya Simba kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Kahata amekuwa mchezaji wa kufanya mazoezi tu kwani hawezi kutumika kwenye ligi na michuano ya kombe la FA
Nyota huyo mkataba wake uko ukingoni, hatma yake ikibaki mikononi mwa mabosi
Uongozi wa Simba unasubiri mapendekezo ya kocha Didier Gomes kuhusu nyota huyo na wachezaji wengine ambao mikataba yao inamalizika
Lakini ni wazi nafasi ya Kahata kubaki Simba ni ndogo hasa kutokana na mchango wake mdogo msimu huu
Baada ya Simba kumsajili Perfect Chikwende ni kama kiungo huyo hana nafasi ya kupata mkataba mpya
ADVERTISE HERE