Simba yajipanga kusaka udhamini mnono

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 May 2021
Simba yajipanga kusaka udhamini mnono

Juzi Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez aliwawakilisha mabingwa hao wa nchi kupokea bonus ya Tsh Milioni 50 kutoka kampuni ya Sportpesa ambao ndio wadhamini wakuu wa klabu ya Simba

Sportpesa walianza kuidhamini Simba msimu wa 2016/17 mkataba wao ukitarajiwa kufika mwisho msimu ukimalizika

Akizungumza katika hafla hiyo, Barbara alisema klabu ya Simba imepanda thamani hivyo wanatarajia kupokea ofa nono zaidi pale mkataba utakapomalizika

Simba imekuwa ikipokea takribani Tsh Bilioni moja kwa mwaka, fedha za udhamini kutoka Sportpesa

Hata hivyo ni wazi Simba inaweza kuachana na Sportpesa kama hawataongeza mkwanja zaidi

"Juzi tumeona Azam Media na TFF wakisaini mkataba mnono wa haki za matangazo ya televisheni. Simba imepanda sana thamani hivyo tunatarajia mkataba mnono zaidi," alisema Barbara

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji aliwahi kudokeza kuwa Simba hairidhishwi na fungu wanalolipwa na Sportpesa hivyo wanaweza kungalia udhamini kwingine kwenye maslahi zaidi

Hivi karibuni Simba ilitoa tenda ya kutengeneza na kusambaza jezi kwa kampuni ya VunjaBei ambayo thamani yake ni Tsh Bilioni 2 kwa mwaka

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
55m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’