Jana klabu ya Kaizer Chiefs ilitangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu Gavin Hunt
Gunt amefutwa kazi siku chache tu baada ya kuchezea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika
Chiefs walinusurika na come-back ya kibabe kutoka kwa Simba ambapo ushindi wa mabao 4-0 waliopata nyumbani uliwasaidia
Lakini Simba ilikaribia kupindua meza katika mchezo uliopigwa jijini Dar es slaam ambapo walitawala kuanzia dakika ya kwanza

Wadau wa Kaizer Chieefs nchini Afrika Kusini waliiponda timu yao licha ya kuingia nusu fainali, baada ya kuzidiwa sana na Simba katika michezo yote miwili
Aidha Simba iliwapoteza kabisa Chiefs kwenye mchezo wa pili jambo lililowaongezea hasira mashabiki wa timu hiyo na kushinikiza atimuliwe
Hunt ni kocha mwingine aliyetimuliwa baada ya kipigo kutoka kwa Simba. Nasreddine Nabi aliyetua Yanga hivi karibuni, nae alitimuliwa Al Merrikh baada ya kushindwa kupata ushindi dhidi ya Simba nchini Sudan
Nabi aliinoa Al Merrikh kwa miezi mitatu tu. Walipokuja nchini, nao walichezea kichapo cha mabao 3-0