Mabingwa wa nchi Simba wako wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi ambapo jioni ya leo majira ya saa kumi, watashuka katika uwanja wa Majaliwa kuikabili Namungo Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya robo fainali, Simba imerejea kwenye mashindano ya ndani kwa nguvu ikipania kutetea mataji yake mawili inayoyashikilia i.e taji la ligi kuu na FA
Tayari wababe hao wa soka Tanzania wametinga nusu fainali ya kombe la FA, leo wanarejea kwenye ligi wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 61 pamoja na mechi nne za viporo
Kiporo cha chanza ni hiki cha Namungo, hesabu zikiwa kukusanya alama zote tatu
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema wanahitaji kushinda mchezo wa leo na utakaofuata dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kwenda mapumziko ya kalenda ya FIFA
Simba iliwasili jana ikiwa na kikosi imara licha ya kuwakosa Clatous Chama, Joash Onyango na Ibrahim Ame
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili Alasiri