Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Jumamosi katika uwanja wa Majaliwa, nyota wawili wa kikosi cha kwanza hawatakuwa sehemu ya mchezo huo
Matola amewataja beki Joash Onyango na kiungo Clatous Chama kuwa watakosekana kwenye mchezo huo
Onyango bado hajapona sawasawa majeraha aliyopata kwenye mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs wakati Chama hakuambatana na timu kutokana na matatizo ya kifamilia
Simba iliwasili Ruangwa mapame leo wakitokea Mtwara walikotua na ndege na kisha kutumia usafiri wa barabara hadi Ruangwa
Matola amesema wachezaji wengine wako tayari kwa mchezo huo
ADVERTISE HERE