Huyu Kagere ni habari nyingine

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 May 2021
Huyu Kagere ni habari nyingine

Jana katika mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Dodoma Jiji, mshambuliaji Meddie Kagere alihitaji dakika tano tu kufunga bao lake la tatu katika michuano hiyo msimu huu

Kagere aliweka kambani bao la tatu kwa Simba katika mchezo huo ambao Simba ilijihakikishia kutinga nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-0

Bado wengi wanajiuliza kwa nini Kagere sio mshambuliaji chaguo la kwanza katika kikosi cha kocha Didier Gomes?

Ukiangalia takwimu, Kagere yuko mbele ya washambuliaji wenzake John Bocco na Chris Mugalu

Msimu huu Kagere amefunga jumla ya mabao 14. Kwenye ligi amefunga mabao 11 na kombe la FA 3

Yuko nyuma kwa mabao matatu dhidi ya kinara wa ufungaji ligi kuu ya Vodacom Prince Dube aliyefunga mabao 14

Hata hivyo Simba ina takribani mechi nne za viporo hivyo ni wazi kama Kagere atapewa nafasi mara kwa mara, anaweza kurejea juu kileleni katika mbio za ufungaji bora

Huu ni msimu wa tatu mfululizo Kagere anawania ufungaji bora. Misimu miwili ameikuba na kiatu cha dhahabu, msimu huu pia ana nafasi kuondoka na kiatu cha dhahabu

Kwa mwendelezo wake wa kuzifumania nyavu, anaweza kumpa sababu Gomes kumuamini na pengine kumtumia mara kwa mara

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’