Hodihodi nusu fainali kombe la FA, Mnyama anataka njia...!
Ni baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa robo fainali uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Simba imerejea na moto waliomaliza nao ligi ya mabingwa wakipata ushindi mwingine wa mabao matatu kwa Mkapa
Ukikutana na Simba hii hakuna mjadala wa ushindi, kinachohesabiwa ni idadi ya mabao ambayo utapigwa
Leo Dodoma Jiji wamepewa dozi ya kutwa mara tatu, imewatosha!



Nahodha John Bocco ameendeleza pale alipoishia mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs akiweka kambani mabao mawili huku bao la tatu likifungwa na 'Bull Striker' Meddie Kagere ambaye wala hana habari na hayo yanayoendelea nje ya uwanja
Ni ushindi ulioipeleka Simba nusu fainali ikikaribia kutetea taji la FA kwa msimu wa pili mfululizo
Katika hatua ya nusu fainali Simba itakutana na Azam Fc kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma