Saa moja usiku leo Jumatano, May 26 Simba itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Mabingwa hao watetezi wamepania kuendeleza pale walipoishia wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa hatua ya 16 bora
Huenda leo washambuliaji Meddie Kagere na Ibrahim Ajib wakajumuishwa katika kikosi kinachoanza
Nyota hao wote wamefunga mabao mawili kwenye michuano hiyo msimu huu
Simba inawania kutinga nusu fainali ambapo katika hatua hiyo itachuana na mshindi wa mchezo kati ya Rhino Rangers dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kuanzia saa kumi jioni
ADVERTISE HERE