Simba imekamilisha ushiriki wake wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu wakifanikiwa kufikia rekodi ya robo fainali kama walivyofanya misimu miwili iliyopita
Katika kampeni ya michuano hiyo, Simba imefunga jumla ya mabao 17, kiungo Clatous Chama akiongoza kwa kupachika mabao matano
Luis Miquissone na John Bocco wamefunga mabao matatu kila mmoja wakati Chris Mugalu ameweka kambani mabao mawili
Nyota wengine waliofunga bao moja ni Larry Bwalya, Mohammed Hussein, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni
ADVERTISE HERE