Simba yarejea mazoezini kuiwinda Dodoma Jiji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 May 2021
Simba yarejea mazoezini kuiwinda Dodoma Jiji

Mabingwa wa nchi Simba jioni ya leo wamerejea mazoezi kujiandaa na mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya kuondoshwa hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba inarejea kwa nguvu kwenye michuano ya ndani kutetea mataji yake mawili

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wanarejea kwenye michuano ya ndani wakiwa na morali ileile waliyomaliza nayo katika michuano ya ligi ya mabingwa

"Tulikuwa na malengo makubwa ya kuingia nusu fainali ligi ya mabingwa lakini bahati haikuwa upande wetu. Kila mmoja ameona vile tulivyopambana. Timu imerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Dodoma Jiji"

"Morali ya wachezaji iko juu, kila mmoja yuko tayari kwa mchezo huo. Hatuwezi kuwadharau wapinzani wetu kwani nao watakuwa 11 uwanjani kama tutakavyokuwa sisi hivyo tunajiandaa kikamilifu," alisema Rweyemamu

Huenda Kocha Didier Gomes akafanya mabadiliko ya kikosi chake siku ya Jumatano akitarajiwa kuwapa mapumziko baadhi ya nyota ambao wamecheza mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’