Gomes aahidi makubwa msimu ujao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 May 2021
Gomes aahidi makubwa msimu ujao

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema ushiriki wao katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, umewafunza nini wanapaswa kufanya msimu ujao ili waweze kufika mbali zaidi

Simba imeondoshwa na Kaizer Chiefs hatua ya robo fainali licha ya ushindi wa mabao 3-0 nyumbani

Kipigo cha mabao 4-0 Afrika Kusini ndicho kilichovuruga hesabu za Simba kwani mabingwa hao wa nchi walipaswa kushinda zaidi ya mabao manne ili kutinga nusu fainali moja kwa moja

Gomes amekiri matokeo ya mchezo wa Afrika Kusini yamechangia kwa kiasi kikubwa wao kushindwa kuvuka hatua ya robo fainali

Hata hivyo hilo ni somo kwao ambapo ameahidi kuwa msimu ujao hawatarudia makosa

"Tulikuwa na malengo ya kutinga nusu fainali lakini imeshindikana. Tumejifunza na tukipata nafasi ya kushiriki msimu ujao tutakuwa bora zaidi," alisema Gomes.

"Wachezaji walipambana kwa ajili ya timu, walifanya kila kitu kwa ajili ya timu lakini bahati haikuwa upande wetu kwa kweli najivunia kufanya nao kazi"

Simba inarejea katika kampeni ya kutetea mataji yake mawili, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam

Keshokutwa Jumatano Simba itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Dodoma Jiji ukiwa ni mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
17h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’