Simba imefunga hesabu zake za ligi ya mabingwa msimu huu kibabe kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs hapo jana
Nyota watano kutoka kikosi cha Simba, wamejumishwa kwenye kikosi cha wiki cha michuano hiyo
Kwa hakika huu umekuwa msimu mzuri sana kwa Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa
Ni bahati mbaya sana hesabu hazikutimia kwa Simba kuingia nusu fainali, lakini vijana wa Didier Gomes walistahili kusonga mbele na pengine hata kufika fainali
Kilichotokea ni matokeo ya mpira wa miguu tu, matokeo hayo hayawezi kuficha ubora ulioonyeshwa Simba

ADVERTISE HERE