Gumzo sio Simba kutolewa michuano ya ligi ya mabingwa, gumzo ni uwezo wa juu ambao Simba imeonyesha kwenye mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs jana
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, ulishuhudia Simba ikipata ushindi wa mabao 3-0 wakiwa pungufu ya bao moja tu kuweza kupindua matokeo ya mchezo wa kwanza ambao walipoteza kwa mabao 4-0 Afrika Kusini
Ni moja ya michezo ambayo Simba ilikuwa katika ubora wake hasahasa. Ukipita kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu ya Kaizer Chiefs, utakubali mashabiki wao wanashangaa timu yao iliweza kuvuka vipi?
Walizidiwa kila idara kwa dakika zote tisini za mchezo, Simba itajilaumu kwa kuruhusu idadi kubwa ya mabao kwenye mchezo wa kwanza, lakini kwa mchezo wa jana hakuna mwenye lawama
Wachezaji walipambana kwa muda wote, wakati mwingine bahati inahitajika kuweza kupata matokeo kwani ni mechi ambayo Simba ingeweza kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao