Simba imekamilisha ushiriki wake wa michuano ya Kimataifa msimu huu hapo jana kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs
Simba sasa inarejea nyumbani kukamilisha kazi iliyobaki, kushinda mataji yote
Jumatano mabingwa wa nchi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Dodoma Jiji ukiwa ni mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam
Baada ya kukosa nafasi ya kutinga nusu fainali ligi ya mabingwa, mnyama atamaliza hasira zake hapa nyumbani
Hao wanaoshangilia Simba kutolewa wajiandae kisaikolojia, Julai 03 sio mbali, labda wakimbie tena
Na hilo likitokea naamini TFF watawashughulikia kwa mujibu wa kanuni za soka
Hii ndio mechi kubwa zaidi iliyobaki msimu huu. Na wakati huo Simba itakuwa tayari imeshatangaza ubingwa
Jana Simba imedhihirisha pasipo na shaka kuwa ni moja ya klabu bora sana barani Afrika wakati huu