Winga wa Simba Barnard Morrison amesema kuwa anajivunia kuwa mchezaji wa Simba licha ya kuwa hawakufanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Jana Simba iliifumua Kaizer Chiefs mabao 3-0 katika mchezo ambao hakika wengi waliridhika na kile kilichofanywa na wachezaji wa Simba
Morrison alikuwa sehemu ya wachezaji waliocheza mchezo huo akiingia kwenye dakika ya 25 kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin
'Mzee wa kuwakera' alifanya kazi yake vyema uwanjani na hata baada ya mchezo alieleza kufurahia kile ambacho yeye na wenzake walikifanya uwanjani katika mchezo huo
"Ninajivunia sana kuwa na jezi hii ya Simba sababu nina furaha. Simba hailingani na klabu yoyote Tanzania, tutashinda makombe yote yaliyobaki. Timu nyingine haziwezi kucheza Kimataifa bila ya Simba"
"Nafikiri Simba itaendelea kuwakilisha Tanzania kwa miaka 15 hadi 20 ijayo..," alisema Morrison