Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes ameeleza kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji kwenye mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, ulishuhudia Simba ikicheza kufa na kupona na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
Simba imeshindwa kutinga nusu fainali kwani ilipaswa kushinda kwa zaidi ya mabao manne
Gomes amesema ni bahati mbaya vijana wake hawakuweza kutinga nusu fainali lakini wamepambana
"Nawapongeza wachezaji wangu, wamepambana kwa muda wote wa mchezo, bahati mbaya hatukuweza kufunga mabao zaidi kutuvusha hatua hii"
"Pengine tulipaswa kuwa makini katika mchezo wa kwanza Afrika Kusini, lakini hata leo tulitengeneza nafasi nyingi, tumefanikiwa kufunga mabao matatu"
"Tulistahili kuvuka hatua hii lakini ni bahati mbaya kwetu," alisema Gomes
Nae nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein amewapongeza wachezaji wenzake kwa jitihada walizoweka katika mchezo wa leo
"Ahsanteni sana wapambanaji wenzangu tumeonesha thaman ya kuvaa jezi ya Simba. Tumeonesha ukubwa wa Simba, haikuwa rahisi ila tumepambana mpaka tone la mwisho Ahsanteni mashabiki zetu nyie ni watu muhimu kwetu. Inshaallah Next time tutakuwa bora zaidi"