Chama, Miquissone, Larry wabeba matumaini ya Wanamsimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 May 2021
Chama, Miquissone, Larry wabeba matumaini ya Wanamsimbazi

Wakati wakihitaji kupata ushindi wa zaidi ya mabao manne dhidi ya Kaizer Chiefs leo, Simba inawahitaji sana Clatous Chama, Luis Miquissone na Larry Bwalya kuwa katika ubora wao

Nyota hawa wametengeneza 'utatu' ambao kama uko katika ubora hakika hakuna wa kuwazuia

Miquissone aliweza kufunga mabao katika michezo mitatu ya hatua ya makundi iliyopigwa jijini Dar es salaam dhidi ya Al Ahly, AS Vita na Al Merrikh

Chama na Bwalya wakahusika katika michezo dhidi ya AS Vita na Al Merrikh

Nyota hawa wanaweza kuamua Simba ichezeje leo, wataamua Simba ishinde mabao mangapi, wataamua kama mashabiki wa Simba leo watarejea nyumbani wakiwa na furaha au huzuni

Aidha, ni mchezo ambao pengine unatamani kumuona uwanjani winga Bernard Morrison ili kuwaongezea presha walinzi wa Kaizer Chiefs

Pamoja na uwepo wa utatu huo, Morrison ni mchezaji wa kipekee anayeweza kukimbia na mpira na kulazimisha walinzi kufanya makosa

Hii ni aina ya michezo ambayo Morrison anaimudu na husababisha madhara

Morrison pia amewahi kucheza soka Afrika Kusini hivyo anayo faida ya kuwafahamu Kaizer na utamaduni wa soka lao

Nyota hawa wataongeza chachu tu, ukweli ni kuwa kila mchezaji wa Simba atakayepewa nafasi ya kucheza leo, anapaswa kujitoa kwa asilimia 100

Safu ya ulinzi inapaswa kuongeza umakini, kwani Kaizer wao watakuwa wakitafuta bao moja tu ambalo linaweza kuvuruga hesabu za Simba

Kaizer wakifunga bao Simba italazimika kushinda kwa mabao sita, hivyo umakini katika ulinzi utahitajika sana

Paschal Wawa, Joash Onyango, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein, wamejifunza kilichotokea Afrika Kusini leo hawapaswi kuwapa nafasi wachezaji wa pembeni kupiga krosi kwani Kaizer silaha yao kubwa ni mipira hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’