Uongozi wa Simba umetangaza utaratibu ambao mashabiki watautumia kukaa majukwaani katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mpaka sasa ni mashabiki 10,000 walioruhusiwa na CAF kuingia 'kwa Mkapa' kushuhudia mchezo huo
Taarifa iliyotolewa na Simba imebainisha kuwa mashabiki wanapaswa kuachiana siti tatu ili kuepuka kuvunja kanuni za corona zilizowekwa na CAF
Tanzania ni nchi pekee barani Afrika ambayo CAF wanaruhusu mashabiki wengi kuingia uwanjani kutokana na kutokuwa na maambukizi makubwa ya corona
ADVERTISE HERE