Tuko tayari kufanya maajabu - Gomes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 May 2021
Tuko tayari kufanya maajabu - Gomes

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema wako tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Gomes amesema wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo, akiamini kuwa hakuna jambo lisilowezekana kwenye mpira wa miguu

Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kuwa wamekusudia kufanya maajabu akiwataka mashabiki wa Simba kuwa na imani, kesho ni siku ya furaha kwao

"Tumefanya maandalizi ya kutosha tayari kuwakabili Kaizer Chiefs. Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi lakini lazima tucheze kufa na kupona. Wachezaji wapo tayari kupambana, wapo tayari kufanya maajabu, hakuna kinachoshindikana," alisema Gomes

Simba inahitaji kupata ushindi wa mabao 5-0 kuweza kutinga nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni baada ya kupoteza kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Afrika Kusini wiki iliyopita

Kwa hakika ni ama zao ama zetu, hii ni vita iliyokamilika, wanajeshi wetu wako tayari kwa mapambano

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’