Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amepania kwelikweli kuwavusha mabingwa hao nchi nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika akiwaandaa vijana wake kuibuka na ushindi wa mabao matano au zaidi dhidi ya Kaizer Chiefs
Ilikuwa wiki ya kazi kazi kwa wachezaji wa Simba waliojichimbia kambini kuhakikisha wanarekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita ambao waliruhusu mabao manne ugenini
Gomes amekuwa mkali zaidi kwa walinzi wake kuhakikisha hawafanyi makosa waliyoyafanya kule Afrika Kusini na kuruhusu kufungwa mabao matatu ya aina moja
Silaha kubwa ya Kaizer Chiefs ni mipira ya krosi kutokana na washambuliaji wao kuwa warefu
Gomes amewaongezea wachezaji wake mbinu katika kukabiliana na mipira hiyo ya krosi
Katika program zake za mazoezi, Gomes alitenga muda kwa ajili ya wachezaji kufanya mazoezi ya mipira ya kichwa
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi, lakini Simba ina dhamira ya dhati ya kupata ushindi mnono kwenye ardhi ya nyumbani
Kama wao walifunga mabao manne kwao, basi hapa Tanzania wanaweza kufungwa na Simba mabao zaidi ya hayo pia
Kama Wydad Athletic waliweza kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs kule Morocco kwa nini Simba wasiweze?