Ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 20 imeendelea leo Jumamosi kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti.
Moja ya michezo hiyo ni uliozikutanisha Azam FC dhidi ya Singida United miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kuzipa changamoto Simba na Yanga katika mbio za ubingwa.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi umemalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Hii ni mara ya tatu kwa Azam FC kukutana na Singida United ambapo imeshinda mara mbili na kutoka sare mara moja.
Ushindi huo umeifanya Azam FC ifikishe alama 38 lakini inabakia nafasi ya tatu nyuma ya Yanga yenye alama 40 nafasi ya pili na Simba iliyo kileleni ikiwa na alama 46.
Mapema, Njombe Mji 'iliipapasa' Ruvu Shooting ya Masau Bwire kwa kuilaza mabao 2-1 huku mchezo kati ya Prisons dhidi ya Mbao FC ukivunjika kwenye dakika ya 50 baada ya mvua kubwa kuharibu mandhari ya dimba la Sokoine.
Mchezo huo ulivunjika wakati Prisons ikiongoza kwa bao 1-0 na utandelea dakika 40 zilizobaki kesho Jumapili asubuhi.
Kagera Sugar nayo imezinduka baada ya kuilaza Majimaji mabao 2-1

ADVERTISE HERE