Nyota Simba wapania kuandika historia Jumamosi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 May 2021
Nyota Simba wapania kuandika historia Jumamosi

Kuelekea mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa Jumamosi, May 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, wachezaji wa Simba wamepania kupambana kufa na kupona kupata matokeo

Jana waandishi wa habari walipewa nafasi ya kufanya mahojiano na wachezaji na benchi la ufundi kuelezea mkakati wao kuelekea mchezo huo

Nahodha wa mabingwa hao wa nchi John Bocco alisema, wao kama wachezaji watahakikisha wanapambana kupata matokeo katika mchezo huo ili waweze kutimiza malengo.

Bocco aliwahakikishia wanahabari kuwa mchezo huo watapigana kadri ya uwezo wao wapate matokeo akiamini lolote linaweza kutokea 

"Kila timu inahitaji matokeo katika mchezo huo, na sisi kama wachezaji ni jukumu letu kuhakikisha tunapambana kupata matokeo ambayo yatazidi kutuweka katika sehemu nzuri maana tukipoteza huo mchezo ndio tumeondolewa, katika kutimiza malengo,"amesema Bocco

Aidha mkongwe Erasto Nyoni alisema watatumia mchezo huo kufuta machungu ya kipigo cha mabao 4-0 walichokipata kutoka mchezo uliopita na muhimu zaidi wanahitaji kutinga nusu fainali

"Tutahakikisha tunapambana kupata matokeo ambayo yatatufanya kutimiza malengo tuliyoyapanga toka mwanza mwa michuano hii, wanasimba waendelee kutusapoti sisi wachezaji tutahakikisha tunapambana kupata matokeo"

Leo Simba inaendelea na mazoezi katika uwanja wake wa Mo Simba Arena lakini siku ya leo waandishi wa habari wamzuiliwa kuingia eneo la uwanja baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na benchi la ufundi na wachezaji hapo jana

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’