Kocha MKuu wa Simba Didier Gomes amesema kikosi chake kina kila sababu ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs
Simba inapaswa kupata ushindi wa angalau mabao matano ili kuweza kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo
Gomes amesema wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita ambao waliruhusu mabao manne kule Afrika Kusini
"Nimetizama mchezo wetu uliopita mara mbili, tulicheza vizuri, timu ilizuia vyema tulijitahidi kuziba nafasi changamoto pekee iliyotusumbua ni mipira ya juu. Tuliruhusu mabao matatu yaliyotokana na mipira ya juu, tumezingatia kutatua changamoto hiyo"
"Nawaambia mashabiki wa Simba, hakuna lisilowezekana. Tunajiamini, tunaamini tunaweza kushinda Jumamosi," alisema Gomes kwenye mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Mo Simba Arena jana jioni
Kuelekea mchezo huo ambao utapigwa saa kumi kamili alasiri, Simba imekuja na kauli mbiu ya 'Ama zao ama zetu do or die season 2'