Manara ataja viingilio mchezo wa Simba vs Al Masry

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Mar 2018
Manara ataja viingilio mchezo wa Simba vs Al Masry
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amezungumza na waandishi wa Habari Leo Makao Makuu ya klabu ya Simba jijini Dar es salaam.

Mbali na mambo mengine, Manara ametaja viingilio vya mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba dhidi ya Al Masry unaotarajiwa kupigwa Jumatano ijayo, March 07 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 12 kamili jioni.

Manara ametaja viingilio hivyo kuwa, mzunguuko ni Tsh 5,000/- huku VIP B ikiwa Tsh 15,000/- na VIP A ni Tsh 20,000/-

Manara amesema wamesogeza mbele muda wa kuanza mchezo huo ili kuwapa nafasi mashabiki wengi waweze kuhudhuria.

Kikosi cha Al Masry kinatarajiwa kutua nchini Kesho Jumapili ambapo kitafanya mazoezi jioni Jumatatu katika uwanja wa Taifa.

Manara amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ili kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa kwanza na kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa March 16 nchini Misri.

Amewataka mashabiki kusahau matokeo ya sare ya jana ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Stand United kwani mchezo wa mpira wa miguu una matokeo matatu, kufungwa, kushinda au kutoka sare.

Amesema matokeo hayo hayamaanishi kuwa Simba haitaweza kutwaa ubingwa kwa kuwa bado iko kileleni mwa msimamo wa ligi.

Amewataka mashabiki wa Simba kuacha kuumizwa na historia ya mwaka jana kwa kuwa historia zipo kwa ajili ya kuvunjwa.

"Miaka ya nyuma tumewahi kuchukua ubingwa tukitoka nafasi ya nne baada ya timu tatu zote zilizokuwa mbele yetu ikiwemo Yanga kufungwa kwenye michezo yao ya mwisho," amesema Manara.

"Hata hao Yanga wamewahi kukosa ubingwa licha ya kuongoza kwa tofauti ya alama 12 ikiwa imebaki michezo sita baada ya kupoteza michezo minne."

Wakati huo huo Manara amethibitisha kuwa nahodha John Bocco na mshambuliaji Emanuel Okwi walipumzishwa tu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Stand United.

Manara amesema kwa kuwa wawili hao ndio kwanza wamepona majeraha yao, benchi la ufundi liliona ni vyema kuwapa mapumziko ili waweze kuwatumia kikamilifu kwenye mchezo dhidi ya Al Masry Jumatano ijayo
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
57m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’