Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amewaongezea wachezaji wake 'dozi' ya mazoezi ili kuhakikisha wanakuwa tayari 'kupindua meza' dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa mkondo wa pili, robo fainali ya ligi ya mabingwa ambao utapigwa Jumamosi
Baada ya kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Afrika Kusini, Gomes alisema wanayo nafasi ya kupata matokeo nyumbani hata hivyo yapo mambo ambayo wanapaswa kuyafanyia kazi haraka
Simba ilianza mazoezi kulekule Afrika Kusini na waliporejea juzi walipewa mapumziko kwa saa kadhaa na jana asubuhi wakarejea mazoezini
Mabingwa hao wa nchi jana walifanya mazoezi asubuhi na jioni, wakijifua kwa masaa matatu kwa kila awamu, program hiyo wakiendelea nayo siku ya leo
Ni mchezo mgumu ambao kwa hakika unahitaji maandalizi ya kipekee. Simba imedhamiria kwelikweli kufuzu nusu fainali