Misimu miwili nyuma katika michuano hii ya ligi ya mabingwa, Simba ilihitaji kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nkana Fc ya Zambia
Mchezo wa kwanza Simba ilifungwa mabao 2-1 kule Zambia na mabingwa wa nchi walihitaji ushindi wa bao 1-0 kuweza kutinga makundi
Katika mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam, Simba ilijikuta nyuma mapema tu kwa bao lililofungwa na Walter Bwalya ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Al Ahly
Hapo mnyama akahitajika kupata ushindi wa angalau mabao matatu kuweza kutinga makundi
Kazi hiyo waliifanya vyema kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kujihakikishia nafasi hatua ya makundi
Msimu huu pia Simba ilitokea nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Platinum Fc na kupata ushindi wa mabao 4-0 hapo kwa Mkapa na kutinga makundi
Jumamosi ya wiki hii May 22, Simba inakabiliwa na mtihani mwingine wa kupindua matokeo katika mazingira tofauti
Kazi inaonekana kuwa kubwa kulinganisha nyakati zilizopita kwani wanahitaji kushinda zaidi ya mabao manne kuweza kutinga nusu fainali
Hakuna jambo lisilowezekana! inawezekana kabisa Simba kushinda mabao matano dhidi ya Kaizer Chief na kutinga nusu fainali
Historia ya Simba miaka ya nyuma, imewahi kufungwa mabao 4-0 hapa nyumbani dhidi ya timu kutoka Msumbiji na wakaweza kushinda mabao 5-0 ugenini
Hii ni aina ya mechi kubwa ambazo Simba imejijengea utamaduni wa kuzicheza vyema uwanja wa Benjamin Mkapa
Hakuna namna, Kaizer Chiefs hawatatoka salama hapo kwa Mkapa, 'ni ama zao ama zetu'