Uwekezaji wa MO Simba waiva

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Mar 2018
Uwekezaji wa MO Simba waiva
Klabu ya soka ya Simba imesema kuwa iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mazungumzo na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji "Mo" kwa ajili ya kuwekeza katika klabu hiyo yenye makao yake makuu Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini, Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah, alisema kuwa Mo ameridhia maelekezo mapya yaliyotolewa na serikali ambayo yanahitaji mwekezaji apewe kiasi cha asilimia 49 na wanachama wabakie na asilimia 51.

Salim alisema kuwa katika kuhakikisha zoezi hilo linakwenda vizuri, tayari wameshasaini mikataba ya awali ambayo inapelekea kurahisisha mchakato huo ambao utabadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1936.

"Tumefikia hatua nzuri katika mchakato huu, kuna baadhi ya nyaraka ambazo zimeshasainiwa, lakini kwa sasa macho na masikio yetu yako kwenye kuelekeza nguvu katika mechi ngumu zinazotukabili," alisema kwa kifupi Salim.

Kuhusu suala la uwanja, kiongozi huyo ambaye alikutana na waandishi wa habari jana asubuhi alisema kuwa wanatarajia kuzipata nyasi bandia zilizokuwa zimezuiwa bandarini wakati wowote kuanzia sasa na mchakato wa ujenzi utaanza hivi karibuni.

Nipashe
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’